Ile msimu ya jafati na nyagus imeround. Naona hulka apa kule zinagwaan katika ile harakati ya kukula shine, kushompa na masafa. Blanda ni ati, hii ni shughuli ya wale wako na maziwa yani cheddars. Ukweli ni ati kama huna hela unabaki kwa mataa yaani mapenzi mtamazaji. Kuna wale wako na sherehe kwenye mahesabu, halafu kuna hawa wanaeka hesabu yote kwa sherehe. Hawa raiyaa wawili wote watajibamba size yake, lakini masaibu itakam mwisho wa risto. Huyu raia alieka hesabu yote kwa sherehe tajipiga kitu baada ya krisi, kawaida ya huyu man wa sherehe kwenye hesabu ni ati, bado meseto zake ziko timam. Si unamezea!
Lazima uwe na mpango kwa kila kitu. Ukipeleka vitu tara ju ya pupa ya krisih budaa utacheza flat jo! Katika hii msimu sio mbaya kuchambua marothi kadhaa ukule shine, kama unachora hivo ngwatha pia ni rada safi. Kupiga sherehe moja mbili na maarif ama mbare pia inaeleweka. Makosa ni wale raiyaa uminya mshiko yote umezunda juu ya pupah za Krisih. Tukubaliane kitu jamo, maisha itaendelea afta krisi,unaona? Usicheze blind ju ya siku kadhaa uharibu siku za usoni.
Naskia mjango anaeza ingia ondira kuwapona ndo krisii im’bambee. Hio ni uwaganis! Piga hesabu, ukishandwa na mabeast ama uende ndonyo future yako imekatsika, ama? Kuzidisha naskia adi mroroo anaeza toka kizee wake juu hana kanyamo wanaeza bonya krisimasi. Bana tukue wapole yo, haina haja udis mtu wako ama hata famee ju ako chupri desemba. We jua, maisha itasonga baada ya krisih. Mtu mjanja anafaa aache pupa, cheze chini hii mwaka enengi uanze meseto mapema ndo hio krisi itafuata ikunaic. Hata hivo, yote tisa ya kide ni ati, usisahau kushukuru Jahjare ata kama huna maweng kumbuka amekugei life. Alhamdulillah! Wabe!