Sarufi ni sheria au kanuni zinazoongoza matumizi ya lugha yoyote ile.

Kwa hivyo, sarufi ya Kiswahili ni kanuni zinazotawala matumizi ya Kiswahili.

Baadhi ya vipengele vya sarufi ni kama vile:

Sauti

Sauti ni mlio au tamko ambalo linatokana na kule kugusana kwa ala za kutamkia.

Aina za sauti:

Neno/Maneno

Neno ni silabi mbili au zaidi yenye maana.

Aina za maneno:

  • Nomino (N):Ni aina za maneno ambazo zinataja jina la mtu, mahali, vitu. Kwa mfano, Juma, shule, Nairobi n.k.
  • Vivumishi (V) : Ni aina za maneno ambazo hutoa maelezo zaidi kuhusu nomino
  • Vitenzi (T) : Ni aina ya maneno ambayo huonyesha kitendo au hali katika sentensi. 
  • Vielezi (E) : Ni aina ya maneno ambayo hutoa maelezo zaidi kuhusu jinsi kitendo kilivyotendeka; yaani zinaeleza zaidi kuhusu vitenzi.
  • Viwakilishi (W) : Ni aina za maneno ambazo hutumiwa kuwakilisha nomino.
  • Viunganishi (U) : aina za maneno ambazo hutumiwa kuunganisha vipashio mbali mbali vya lugha (kama vile sentensi).
  • Vihusishi (H):  Ni aina ya maneno inayoonyesha uhusiano wa nomino na mazingira yake.
  • Vihisishi (I):  Ni aina za maneno ambazo huonyesha hisia

Sentensi

Sentensi ni fungu la maneno lenye maana kamili.

Aina za Sentensi

Uchanganuzi wa sentensi

Uchanganuzi wa sentensi ni kugawa sentensi katika makundi ya maneno na aina ya maneno.

Ngeli za Kiswahili

Ngeli ni vikundi vya nomino ya Kiswahili.

Zifuatazo ndizo ngeli za Kiswahili:

Viambishi

Viambishi ni maneno yanayoongezwa/ambishwa kwenye mzizi wa neno hili kupea neno hilo maana.

Aina za Viambishi