Viambishi ni maneno yanayoongezwa/ambishwa kwenye mzizi wa neno hili kupea neno hilo maana.
Mzizi ni sehemu ya neno isiyobadilika katika hali yoyote ya unyambuzi. Kwa mfano:
Mfano I
Mzizi wa neno cheza ni chez; kama ilivyo kwenye:
a. cheza
b. chezea
c. chezeshwa
Kutokana na mfano wetu, chez ndio mzizi wa neno cheza kwa sababu haibadiliki hata kwenye unyambuzi tofauti tofauti wa neno ‘cheza’.
Mfano II
Mzizi wa neno rudisha ni rudish; kwa mfano:
a. rudisha
b. rudishwa
c. rudishiwa
Aina za Viambishi
Kuna aina mbili za viambishi:
- Viambishi Awali
- Viambishi Tamati.
Viambishi Awali
Viambishi awali hutokea kabla ya mzizi wa neno. Kwa mfano:
1. Walichezeshwa
Kwenye sentensi hii, mzizi ni chez, kwa hivyo, maneno yote yanayotokea kabla ya chez, ni viambishi awali; hivyo basi, viambishi awali ni:
Wali kwenye wali-chezeshwa.
Viambishi hivi hubeba maana ya kisarufi: Wa-li; wa inarejelea nomino inayozungumziwa; li inarejelea wakati (na katika mfano wetu, li ni wakati uliopita).
Viambishi Tamati
Haya ni maneno yanayoambatanishwa baada ya mzizi wa neno/ yaani hutokea baada ya mzizi wa neno; na pia hubeba maana ya kisarufi.
Tutatumia mfano wetu kuonyesha viambishi tamati
Walichezeshwa
Mzizi ni chez; kwa hivyo maneno yote yanayofuata chez, ni viambishi tamati- eshwa.
Mifano zaidi: