Sentensi ni fungu la maneno lenye maana kamili.
Sentensi huwa ni muundo wa kiima na kiarifa.
Kiima ni sehemu ya sentensi inayotawaliwa na nomino; pia inaitwa Kundi Nomino (KN). Kiima huonyesha ni nomino gani au kiwakilishi chake ambacho hupelekea kutendeka kwa kitendo kwenye sentensi.
Kiarifa inarejelea sehemu ya sentensi inayotawaliwa na kitenzi; pia inajulikana kama Kundi Tenzi (KT).
Kwa mfano: Juma (Kiima)alimpikia Musa chakula kitamu (Kiarifa).
Aina za Sentensi
Kuna aina tatu za sentensi za Kiswahili:
- Sentensi sahili
- Sentensi Ambatano
- Sentensi Changamano.
Sentensi Sahili
Hizi ni sentensi ambazo huwa na kitenzi kimoja kikuu.
Kwa mfano:
- Baba anasoma gazeti.
- Mama anapika wali.
Sentensi Ambatano
Sentensi ambatano huundwa kwa sentensi sahili mbili au zaidi.
Sentensi hizi sahili huunda sentensi ambatano kwa kuletwa pamoja na kiunganishi.
Sentensi Changamano
Sentensi changamano ni aina ya sentensi ambayo huwa na muundo wa vishazi huru na vishazi tegemezi ambazo huunganishwa pamoja na –o ama amba- rejeshi.
Kwa hivyo, sentensi zote ambazo huwa na amba- ama –o rejeshi ni sentensi changamano.
Mifano:
- Watoto waliopotea juzi wamepatikana
Tukiangalia hii sentensi, tunaona –o rejeshi kwenye “waliopotea”. Aidha, tunapata vishazi viwili kutokana na sentensi hii: Kishazi huru > Watoto wamepatikana
Kishazi tegemezi > Waliopotea juzi
- Gari ambalo liliibwa jana limepatikana mtaani.
amba- rejeshi (ambalo)
kishazi huru > Gari limepatikana mtaani
kishazi tegemezi > Ambalo liliibwa jana.
Uchanganuzi wa Sentensi
Uchanganuzi wa sentensi ni kule kugawa sentensi katika makundi ya maneno na aina ya maneno.
Kuna njia tatu za kuchanganua sentensi:
- -Jedwali
- -Mishale
- -Matawi
Tutachanganua sentensi mbali mbali kwa kutumia njia hizi tatu.
Uchanganuzi wa sentensi kwa njia ya Jedwali
Mama alienda sokoni (Sentensi Sahili)
Uchanganuzi wa sentensi kwa njia ya Mishale
Mzee safi atazawadiwa gari (sentensi sahili)
Uchanganuzi wa sentensi kwa njia ya Matawi
Mzee safi atazawadiwa gari