Sauti ni mlio au tamko ambalo linatokana na kule kugusana kwa ala za kutamkia. Sauti huwakilishwa na alama //.
Kwa Mfano, /b/, /d/, /e/ n.k.
Lugha ya Kiswahili huwa na aina mbili kuu za sauti ambazo ni:
- Konsonanti
- Irabu
- Silabi
Konsonanti
Sifa moja kuu ya konsonanti za Kiswahili ni kuwa; sauti hizi zinapotamkwa, hewa hubanwa/huzuiliwa kwenye ala za kutamkia. Kuna aina nyingi za konsonanti kutokana na ala zinazotumika katika kuzitamka na pia jinsi ya kuzitamka.
Konsonanti pia zinaweza ainishwa kutokana na sifa ya ghuna (h) na sighuna (gh). Kutokana na nyenzo hizi tatu, tunapata aina hizi za konsonanti:
Aina Za Konsonanti
*Sauti ghuna (h) ni zile konsonanti ambazo wakati zinapotamkwa, huwa kuna mtetemeko/mtikisiko wa nyuzi za sauti ilhali huwa hakuna mtetemeko wa nyuzi za sauti sauti sighuna (gh) zinapotamkwa.
Irabu
Pia zinajulikana kama vokali. Irabu za Kiswahili ni zile sauti ambazo zinapotamkwa, hewa huwa haizuiliwi/haibanwi kwenye ala za kutamkia.
Kuna aina tano za irabu za Kiswahili: /a/, /e/, /i/, /o/, /u/.
Irabu za Kiswahili huainishwa kwa kutumia vigezo viwili vikuu: sehemu ya ulimi na hali ya mdomo.
Kutokana na kigezo cha sehemu ya ulimi, tunapata irabu za mbele, kati na nyuma.
Sehemu ya Ulimi
Hali ya Mdomo
Kutokana na kigezo hiki, tunapata irabu ambazo hutamkwa wakati midomo imetandazwa k.v /a/, /e/ na /i/.
Vilevile, kunazo irabu ambazo hutamkwa wakati midomo imevirigwa k.v /o/ na /u/.
SILABI
Silabi ni sauti mbili au zaidi zinazotamkwa kwa pamoja au kama sauti moja.
Silabi huwa hazina maana toshelezi. Kwa mfano; /b/ pamoja na /a/ zinaunda silabi ba.
Mifano katika neno: dak-ta-ri; shu-le; ma-ma; muk-ta-dha
Kuna aina mbili kuu za silabi za Kiswahili; silabi funge na silabi huru
Silabi funge/ambata
Hizi ni silabi ambazo huishia kwa konsonanti. Kwa mfano: Dak kwenye daktari; Kab kwenye kabla; Muk kwenye muktadha
Silabi huru/wazi
Silabi huru za Kiswahili ni zile silabi ambazo huishia kwa irabu. Maneno mengi ya Kiswahili huundwa kwa silabi huru.
Kwa mfano: mu kwenye mwa-li-mu; ma kwenye li-ma.