Vielezi huwakilishwa kwa herufi E.
Ni aina ya maneno ambayo hutoa maelezo zaidi kuhusu jinsi kitendo kilivyotendeka; yaani zinaeleza zaidi kuhusu vitenzi.
Kwa mfano; Alifika (T) mapema (E).
Kuna aina nne za Vielezi vya Kiswahili:
Vielezi vya Mahali
Vielezi hivi huonyesha mahali ambapo kitendo kilitendeka.
Kwa mfano:
- Wanafunzi walisoma darasani.
- Wazazi walilima shambani.
- Mama alienda sokoni.
Vielezi vya Wakati
Huonyesha wakati kitendo kilitendeka.
Kwa mfano:
- Mama atarudi jioni.
- Shule zitafunguliwa mwezi ujao.
Vielezi vya Jinsi.
Vinaonyesha namna kitendo kilitendeka.
Kwa mfano:
- Aliingia polepole
- Mzee alifua kivivu
- Wanafunzi walisoma kimoyomoyo.
Vielezi vya Idadi
Vinaonyesha mara ngapi au kiasi kipi kitendo kimetokea.
Kwa mfano:
- Mama hufua mara nyingi.
- Wanafunzi husoma siku zote.