Vihisishi huwakilishwa kwa herufi I.
Ni aina za maneno ambazo huonyesha hisia. Kuna hisia mbalimbali zinazoonyeshwa na vihisishi.
kama vile:
- Huzuni
Kwa mfano: Salale!
- Furaha
Kwa mfano: Shabash! Oyee! Ahaa!
- Mshangao
Kwa mfano: Ala! Aka! Ebo! Masalale!
- Kuakiki/Kukubali
Kwa mfano: Hewaa! Naam!
- Hisia za dharau
Kama vile: Ebo! Po!
Hisia ni nyingi. Vihisishi vinapotumiwa kwenye sentensi, alama ya kihisi (!) hutumiwa.