Vihusishi vya Kiswahili huwakilishwa na herufi H.
Ni aina ya maneno inayoonyesha uhusiano wa nomino na mazingira yake.
Mifano: Kando ya, mbele ya, kabla ya, katikati ya, katika n.k.
Mifano katika sentensi:
- Mama alisimama katikati ya barabara.
- Mtoto alicheza kando ya mto.
- Mwanafunzi alifika kabla ya/mbele ya mwalimu.
- Paka yuko chini ya meza.