Vitenzi huwakilishwa na herufi T.
Ni aina ya maneno ambayo huonyesha kitendo au hali katika sentensi.
Kwa mfano:
- Mama anapika (kitendo)
- Mwalimu ni mgonjwa (hali).
Zifuatazo ni aina mbalimbali za vitenzi vya Kiswahili:
Vitenzi halisi/Vikuu
Huonyesha kitendo halisi au kikuu au muhimu ambacho kinatendwa na mtendaji kwenye sentensi.
Kwa mfano:
- Watoto wanacheza mpira.
- Musa anasoma gazeti.
Vitenzi Visaidizi
Kinasaidiana na kitenzi kikuu ili kufafanua kitendo kikuu au kukifanya kueleweka zaidi.
kwa mfano:
Watoto walikuwa (kitenzi kisaidizi) wanacheza(kitenzi kikuu) mpira.
Vitenzi Vishirikishi
Ni aina za vitenzi ambazo hushirikisha vitu kihali, kitabia au kimazingira
Kwa mfano:
- Maria ni msichana mkorofi; sisi tu wanafunzi wenye msimamo
- Mama yangu si mkali.