Viunganishi huwakilishwa na herufi U.
Viunganishi ni aina za maneno ambazo hutumiwa kuunganisha vipashio mbali mbali vya lugha (kama vile sentensi).
Mifano katika sentensi:
Baba anasoma gazeti. Mama anapika. - Baba anasoma gazeti huku mama akipika.
Kama motto anaweza kusoma, sembuse mimi.
Nitamlipa pesa nyingi kwa sababu alifanya kazi nzuri.
Msichana huyu ni mwerevu tena ni mwenye utu.