Neno ni silabi mbili au zaidi yenye maana.

Kwa mfano; kutokana na silabi hizi mwa-li-mu; tunapata neno mwalimu; vile vile; silabi hizi ba-ra-ba-ra zinaunda neno barabara.

Silabi ma-ma zinaunda neno mama. Kuna aina tofautitofauti za maneno ya Kiswahili:

Aina za Maneno

Lugha ya Kiswahili, kama ilivyo lugha ya Kiingereza, ina aina nane za maneno. Zifuatazo ndizo aina za maneno ya Kiswahili:

Nomino (N)

Ni aina za maneno ambazo zinataja jina la mtu, mahali, vitu.

Aina za Nomino:

  • Nomino za Kawaida
  • Nomino za Kipekee
  • Nomino za Jamii/Makundi
  • Nomino za Kitenzi-Jina
  • Nomino za Dhahania
  • Nomino za Wingi

Vivumishi (V)

Vivumishi ni aina za maneno ambazo hutoa maelezo zaidi kuhusu nomino.

Aina za Vivumishi:

  • Vivumishi vya Sifa
  • Vivumishi vya Idadi
  • Vivumishi Viashiria
  • Vivumishi Vimilikishi
  • Vivumishi Visisitizi
  • Vivumishi Viulizi
  • Vivumishi Virejeshi
  • Vivumishi Vya A-Unganifu
  • Vivumishi Vya KI-Mfanano

Vitenzi (T)

Ni aina ya maneno ambayo huonyesha kitendo au hali katika sentensi.

Aina za vitenzi:

  • Vitenzi halisi/Vikuu
  • Vitenzi Visaidizi
  • Vitenzi Vishirikishi

Vielezi (E)

Ni aina ya maneno ambayo hutoa maelezo zaidi kuhusu jinsi kitendo kilivyotendeka

  • Vielezi vya Mahali
  • Vielezi vya Wakati
  • Vielezi vya Jinsi.
  • Vielezi vya Idadi

Viwakilishi (W)

Viwakilishi ni aina za maneno ambazo hutumiwa kuwakilisha nomino.

Aina za viwakilishi

  • Viwakilishi vya Nafsi
  • Viwakilishi Vionyeshi
  • Viwakilishi Viulizi
  • Viwakilishi Vimilikishi
  • Viwakilishi Virejeshi
  • Viwakilishi vya Sifa
  • Viwakilishi vya Idadi
  • Viwakilishi vya Pekee
  • Viwakilishi vya A-Unganifu

Viunganishi (U)

Viunganishi ni maneno ambazo hutumiwa kuunganisha vipashio mbali mbali vya lugha.

Vihusishi (H)

Vihusishi ni aina ya maneno inayoonyesha uhusiano wa nomino na mazingira yake.

Vihisishi (I)

Vihisishi ni aina za maneno ambazo huonyesha hisia.